30 Juni 2025 - 13:43
Source: Parstoday
Profesa wa Chuo Kikuu cha Georgetown: Msimamo wa Iran wa kutokuwa na imani na Marekani unaeleweka

Shireen Hunter, profesa katika Chuo Kikuu cha Georgetown huko Washington, DC amesema kuwa, mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya Iran yalifanywa kwa lengo la kuvuruga mazungumzo kati ya Tehran na Washington yaliyokuwa na lengo la kupata suluhisho la amani la suala la nyuklia la Iran na kusema: Kutokuwa na imani kwa Iran na nia na malengo ya Marekani kunaeleweka, na Tehran lazima itake dhamana inayohitajika katika makubaliano yoyote yajayo.

 Shireen Hunter ameongeza kuwa: "Iran inapaswa kujumuisha hatua na kutaka dhamana katika makubaliano yoyote ya siku za usoni na Marekani ili isishtukizwe tena kwa mabadiliko ya misimamo ya Marekani, kama ilivyotokea kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA."

Profesa wa Chuo Kikuu cha Georgetown amesema: "Israel haitaki kuwepo maridhiano kati ya Marekani na Iran, na mashambulizi ya Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ni uchokozi na kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa."

Ameongeza kuwa: "Muqawama na utetezi wa Iran wa mamlaka yake ya kujitawala vimeonyesha kuwa vita vitakuwa na gharima hata kwa Marekani."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha